Mpenzi wake DJ Evolve humtembelea na kumsaidia-John Orinda

Muhtasari
  • John Orinda akiwa kwenye mahojiano na radiojambo alifichua kwamba mpenziye DJ Evolve huwa anamtembelea

Kila mtu anapopatwa na shida marafiki wake wa karibu huwa wanamtoroka kutokana na shida zake, lakini kwa mpenzi wake DJ Evolve hajaweza kufanya hayo amekuwa naye kwa vyovyote vile.

John Orinda akiwa kwenye mahojiano na radiojambo alifichua kwamba mpenziye DJ Evolve huwa anamtembelea.

"Kabala ya ajali alikuwa na mpenzi, ambaye huwa anakuja kumuona na kuenda kwa mana anaishi kwake

 
 

Pia amekuwa akimsaidia nyumbani, marafiki zake huwa pia wanakuja kumtembelea baada ya ajali hiyo," Alisema John.

Bwana Orinda alisema kwamba anamshukuru Mungu kwa kuwa mtoto wake yuko hai licha ya awali kukejeliwa kwa kumshukuru Babu Oeino kwa kumpeleka mwanawe hospitali kwa wakati unaofaa.

Pia alifichua ya kwamba huwa wanazungumza na Babu Owino kupitia madaktari.

"Hakururhisiwa na mahakama kumuona DJ Evolve, kama dawa zimeisha huwa tunaambia madaktari wanamwambia na kisha wanatuambia vile amesema

hatukutoa kesi yetu kirtini kama ilivyodaiwa awali kwenye mitandao ya kijamii,"