'Chumbia mwanamume anayeona thamani yako kama mwanamke,'Akothee amwambia mwanawe

Muhtasari
  • Msanii Akothee amshauri mwanawe kwa mambo haya huku akisheherekea siku yake ya kuzaliwa
rue baby
rue baby

Msanii Akothee akimtakia mwanawe siku na heri njema huku akisheherekea siku yake ya kuzaliwa alimwamba aweze kuolewa na wala asibaki kuwa kama mama yake.

Kupitia kwenye ujumbe mrefu kwenye ukurasa wake wa instagram pia msanii huyo alimshauri Rue Baby ya kwamba atie bidii ktika ndoto zake na kuwaheshimu wakubwa wake.

Pia alisema kwamba inachukua tu nidhamu ya mtu ili afike malengo yake.

 

"Chumbia mwanamume anayeona thamani kwako kama mwanamke, mwanamume ambaye atakuheshimu na kukupenda,

Mwanaume ambaye atatunza familia yako, sio kijana wa muda ambaye atakuja na kukata kichwa changu kwa nyinyi kurithi utajiri wangu na kuuza kila kitu,

Mwanaume ambaye hataona anakugeuza kuwa mlango wa mlango, mashine ya pesa au kitu kama hicho Kuoa ikiwa inawezekana usiishie kama mama yako,

uzazi wa moja sio kiburi, ni hali ambayo hakuna mtu anayetabiri, lakini hatujutii, ingawa tunawaonea wivu watu walioolewa na upendo πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Sijui viatu vyao πŸ‘Ÿ Kiatu pekee ninachokijua ni umoja pris πŸ’ͺπŸ’ͺπŸ˜‚πŸ’ͺπŸ’ͺπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚," Aliandika Akothee.

Akothee aliandelea na ujumbe wake na kumwambia kuwa,

"Maoni ya watu juu yako, haipaswi kuwa ukweli wako, Unapaswa kuwa mtu wa mwisho na maoni juu yako mwenyewe. Watu wengi huzungumza nawe nje ya ndoto yako kwa sababu mioyo yao iko tayari lakini miili yao ni dhaifu,"