Mchekeshaji Eric Omondi asema atamlipa Ezekiel Mutua shillingi 750,000 baada ya kufanya haya

Muhtasari
  • Hii hapa sababu ya Eric Omondi kutaka kumlipa Ezekiel Mutua
  • Haya yanajiri punde tu baada ya bosi wa KFCB kupitia ukurasa wake wa twitter kuwaambia watu wawe sawa na kukosolewa
Eric Omondi

Mcheshi Eric Omondi amejitolea kumlipa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Uainishaji wa Filamu Kenya (KFCB) Ezekiel Mutua Sh750,000.

Haya yanajiri punde tu baada ya bosi wa KFCB kupitia ukurasa wake wa twitter kuwaambia watu wawe sawa na kukosolewa na watu wazungumze juu yao, kwa sababu ndivyo maadui wanavyotangaza chapa ya mtu bila kulipia.

“Ridhika na kukosolewa na watu wakiongea juu yako. Ndio jinsi maadui zako wanavyotangaza chapa yako bila wewe kulipa chochote," Aliandika Ezekiel.

 

Baada ya mmoja wa mashabiki wake kumuuliza kama jinsi anamtangaza Eric Omondi, mchekeshaji huyo alipakia ujumbe wake Ezekiel kwenye ukurasa wake wa instagram na kusema kwamba amekuwa akifanya kazi njema.

Na kwa ajili ya hayo atamlipa shillingi 750,000 kwa nzuri.

"Nakubaliana kabisa na wewe Mheshimiwa. Wewe ndiye unaye tangaza kazi zetu katika Nchi hii na ukweli kwamba unaifanya bure huifanya iwe haki kwako

Wewe peke yako uliuza Studio na ofisi zangu kwa kuziita danguro. Kitu ambacho kingegharimu Mamilioni ya shilingi kufanya

Tafadhali ofisi yako initumie Ankara kwa ofisi za Big Tyme Entertainment katika barabara ya Maji Mazuri Lovington.

Ninakuahidi (na unaweza kutegemea neno langu) nitakulipa jumla ya Ksh 750,000," Alisema Omondi.