Hakuna siku moja nitaacha yesu, hata shetani anajua - Ringtone asema

Muhtasari
  • Ringtone asema hamna kitu kinaweza kumtenganisha na Mungu, huku akisema baadhi ya wasanii baada ya kubarikiwa na Mungu waliacha kumuabudu

Msanii Ringtone akiwa kwenye mahojiano alisema hamna kitu hii duniani kinaweza mtenganisha na Mungu.

Huku akijibu madai yake kutoka kwenye tasnia ya usanii kama Mungu hatambariki na gari la aina ya BMW i8 alisema kwamba wanaddamu wanahukumu kwa matamshi ya mtu.

"Ubaya wanadamu huwa wanahukumu mtu kutokana na matamshi yake lakini Mungu huwa anaangalia moyo

 

Wasanii wengi wamekuja kwenye tasnia ya buradani ya nyimbo za injili kisha baada ya kubarikiwa na Mungu wanaacha kumuabudu Mungu

Mimi nko katika tasnia ya nyimbo za injili kwa maana najua na nafahamu vyema mali Mungu amenitoa, kutoka mitaani hadi kunifanya milionea

Kuna wakati nilienda kutafuta bibi, Mombasa lakini nikapata ni wanawake wazee,ata shetani mwenyewe anajua siwezi toka kwa Mungu

Hakuna kitu chochote ambacho kinaweza nitenganisha na Mungu," Aliongea Ringtone.