Mimi sijali wanachosema watu kunihusu-Ringtone aweka mambo wazi

Muhtasari
  • Ringtone aweka wazi hajali wanachosema watu kumhusu
  • Pia msanii huyo alisema Mungu ndiye msema yote na atajali kile Mungu atasema kuhusu maisha yake
ringtone
ringtone

Msanii wa nyimbo za injili Ringtone Apoko mara kwa mara amekuwa akivuma kwenye mitandao ya kijamii kwa ajili ya matamshi yake ya hapa na pale.

Akiwa kwenye mahojiano ingtone alisema kwamba hajali kile watu wanasema kumhusu bali anajali kile Mungu anasema.

"Ninaweza imba nyimbo zipendwe na watu wengi wengi waniandikie jumbe za kunipongeza lakini kama Mungu hajafurahishwa na kitendo changu sijafanya kitu

 

MImi kama msanii wa nyimbo za injili sijali kile watu wanasema bali najali kile Mungu anasema kuhusu maisha yangu

Mimi nitasema leo hadharani kwamba mimi ni milionea, na kama mimi ni milionea azima nyimbo zanu zipate watazamaji zaidi ya milioni,"Alizungumza Ringtone.

Ringtone alisema alikuwa bila ya kupata upendo wa wazazi kwa maana baba yake aliaga dunia akiwa mchanga huku mama yake akimuacha na kuenda.