Karen Nyamu hatimaye amuomba mkewe Samidoh, Edith msamaha

Muhtasari
  • Mwanasiasa wa Nairobi Karen Nyamu kwa mara ya kwanza amemuomba msamaha mke wa mwanamuziki Samidoh Edith kwa kumnyemelea mumewe.
  • Nyamu alisema hamchukiiEddith na hata kuna wakati alimsaidia kupata zabuni ya zaidi ya KSh 900 milioni

Mwanasiasa wa Nairobi Karen Nyamu kwa mara ya kwanza amemuomba msamaha mke wa mwanamuziki Samidoh Edith kwa kumnyemelea mumewe.

Akiwa kwenye mahojiano, siku ya jumatano Karen alisema kwamba alifahamu Samidoh ana mke baada ya kujua kwa miezi 4.

Nyamu alisema hamchukiiEddith na hata kuna wakati alimsaidia kupata zabuni ya zaidi ya KSh 900 milioni.

 

Kulingana na nyamu, Wakenya wameichukulia sarakasi inayoendelea kati yake na familia ya Samidoh visivyo.

Pia mwanasiasa huyo alisistiza kwamba yeye hakuvunja familia yeyote, na alikuwa anataka watu wajue aba ya mtoto wake waache kumkejeli kwenye mitandao ya kijamii.

Alichukua fursa hiyo na kumuomba Eddith msamaha kwa yote ambayo yametokea awali.

" Najutia sana kwa hii sarakasi yote ambayo imetokea, kwa muda huu wote nilijua ulijua si tu eti najitetea lakini naomba radhi,

"Mbona nimchukie mtu ambaye kwa wakati mmoja niliwahi kumsaidia, nilimsaidia akapata zabuni ya zaidi ya KSh 900 milioni ambayo bado anaihudumia, tuliafikiana na kakake Samidoh na tukamsaidia kupata zabuni hiyo," Alisema.

Alichukua fursa hiyo na kumuomba Eddith msamaha kwa yote ambayo yametokea awali.