'Kwa nini msiandike kuhusu biashara zangu,'Vera Sidika akana madai kwamba alianguka jukwaani

Muhtasari
  • Vera Sidika akana madai ya kuanguka jukwaani
  • Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Vera alikana madai hayo na kusema kwamba ana mambo muhimu ya kufanya na wala sio kuwaburudisha watu
Vera Sidika

Wiki iliyopita video ilienea sana kwenye mitandao ya kijamii na kudaiwa kwamba ni mwanabiashara Vera Sidika alianguka akiwaburudisha mashabiki.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Vera alikana madai hayo na kusema kwamba ana mambo muhimu ya kufanya na wala sio kuwaburudisha watu.

Uso wa mwanamke huyo haukuonekana ambapo wanamitandao waliamini kuwa ni Vera Sidika.

 

"Unajua wanablogu hawana kazi, ambapo wanachukua video na kudai kwamba na kuandika ni wewe, ndio watu waweze kusoma ilhali sio wewe

Hamna mtu ambaye atabonyeza kwenye kiungo na kutazama kama ni wewe, mnapaswa kuwa makini na maisha yenu,mnafikiria nina wakati wa kuharibu kwa kuhudhuria sherehe kama hizo

pia mlikuwa na ujasiri wa kuandika kuwa nilikuwa na waburudisha watu, nyinyi ni wagonjwa kwenye vichwa vyenu, kama hamna kazi ya kufanya basi ketini na kutazama nyasi zikimea," Vera aliandika.

Pia alizidi na kunakili ujumbe wake huku akiwashauri waliodai kwamba ni yeye wangeandika kuhusu biashara yake ya saluni.

"Ati Vera Sidika anaanguka jukwaani wakati akiburudisha wageni Je! Ni wavivu? Je, wewe ni kipofu  huwezi kuona mtu yeyote unayedai ni mimi hata haonekani kama mimi!

Au unafikiri nina wakati wote ulimwenguni kuhudhuria hafla kadhaa za kuchekesha na kuanza kuwaburudisha wageni kama unavyodai.

Je, ni kawaida ??? Smh 🤦‍♀️ kwanini siku moja usikae na uandike juu ya spa yangu @ vsspa001 na kazi ya kushangaza tunayofanya.

 

Kwa nini usiandike kuhusu vetox @veetoxdetox na jinsi inasaidia watu kupunguza uzito na kuchoma mafuta ya tumbo. Mtakuwa na nguvu ya kuchora uzembe kwa watu lakini hakuna cha kuwainua !!!,"