Maoni:Je Samidoh anapaswa kuoa wake wengi baada ya drama yake?

Muhtasari
  • Je Samidoh anapaswa kuoa wake wengi,baada ya drama yake?
  • Baada ya kuomba msamaha wengi walimsifu kwa kujitokeza kama mwanamume na kuubali makosa yake
samidoh 3
samidoh 3

Wikendi iliyopita msanii Samidoh amekuwa akivuma sana baada ya mwanasiasa Karen Nyamu kuthibitisha kwamba msanii huyo ni baba wa mtoto wake.

Baada ya siku chache Samidoh aliomba msamaha kwa yote ambayo yalikuwa yametokea.

Baada ya kuomba msamaha wengi walimsifu kwa kujitokeza kama mwanamume na kuubali makosa yake.

 

Karen akiwa kwenye mahojiano alisema kwamba hakujua wala kufahamu kama Samidoh alikuwa ameolewa kwani hakuwa amevalia pete.

Swali kuu ni je Samidoh anapaswa kuoa wake wengi kama watu wengine mashuhuri humu nchini?

Najua kuna wale watapinga na kusema kwamb anapaswa kutosheka na mkewe pekee na pia kuna wale wataunga mkono anapaswa ili asiwe na mipango ya kando.

Je kama unaunga mkono anapaswa kuoa wake wengi au kujiunga na kikundi cha 'polygamous' toa sababu na akama unakataa hapaswi pia toa sababu yako.

Ndio tumewaona wasanii,watu mashuhuri, pia mababu zetu walikuwa wanaoa wake wengi ukipata hatosheleki na mke mmoja.

Na je ni vyema kuwa na wake wengi au ni vyema kuwa na mpango wa kando, lakini mpango wa kando ni kama decoder kama hujalipia huwezi ona au kutazama filamu zako.