Nimekuwa mgonjwa kwa zaidi ya miaka 19, na kukosa kazi kwa miaka 6-Jahmby Koikai

Muhtasari
  • Jahmby Koikai asema amekuwa mgonjwa kwa zaidi ya miaka 19
  • Pia alisema kwamba wakati huo hukumbuka Mungu hutimiza ahadi zake siku zote
Kila siku zake zilipokaribia, alikuwa anapatwa na uchungu mwingi. Picha; JAHMBY KOIKAI.
Kila siku zake zilipokaribia, alikuwa anapatwa na uchungu mwingi. Picha; JAHMBY KOIKAI.

Jahmby Koikai kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amefichua changamoto ambazo amepitia katika maisha yake.

Kupitia kwenye ujumbe wake Jahmby amesema kuwa wakati huo amekuwa akimuuliza Mungu maswali huku kila wakati akiwa na uvumilivu.

Pia alisema kwamba wakati huo hukumbuka Mungu hutimiza ahadi zake siku zote.

 

"Maisha yangu ni ushuhuda mkubwa kwamba Mungu bado yuko katika biashara ya kurudisha watu wake

Nimekuwa mgonjwa kwa zaidi ya miaka 19 na kukaa bila kazi kwa miaka 6 iliyopita

Nimemuuliza Mungu maswali mara nyingi na kila wakati niliongozwa kwa uvumilivu kupitia majibu ya Mungu

Wakati wake unanikumbusha kwamba ahadi Zake hazitowi kamwe,Pia iliniongoza kwenye nafasi ya ibada na uwepo wa Mungu," Aliandika Jahmby.

Jahmby aliwahimiza wale wamo katika hali mbaya kama alivyokuwa, kwamba Mungu yupo nao kwani machozi yao sio ya bure.

"Kuna watu wengi katika nafasi ile ile ya kupambana na magonjwa, ukosefu wa ajira, kukata tamaa, kukosa tumaini, upweke

Machozi yako sio bure. Kile ulichopoteza kitabadilishwa na kitu kikubwa zaidi. Mungu anakuona na kukusikia,"