Caroline Muthoni mpenzi wake Mulamwah akiwa kwenye mahojiano na Radiojambo alisema kwamba wanamitandao wengi walimkejeli sana baada ya mimba yake kutoka mapema.
Muthoni mwaka jana mimba yake ilitoka mapema, huku akisema kwamba hajui sababu ya mimba yake kutoka.
"Hadi leo sijawahi elewa kwanini mimba yangu ilitoka mapema, madaktari waliniambia kwamba nilikuwa na dhiki na ilisababisha mimba yangu kutoka
Nilipokea kejeli nyingi kutoka kwa mashabiki, wengi walikuwa wananiuliza kwanini nilikubali mimba ya Mulamwah ikatoka, ni kama nilikuwa na chaguo
Mulamwah alinipa ushauri baada ya mimba yangu kutoka mapema,mimi naogopa sana kupta ujauzito kwa sababu ya yae yalitokea,"
Caroline na Mulamwah wamekuwa katika uhusiano wa kimapenzi kwa miaka 4.