Usimuache mume wako kwa maana amemuendea mwanamke mwingine-Msanii Loise Kim awashauri wanawake

Muhtasari
  • Msanii Loise Kim awashauri wanawake mambo haya kuhusu waume zao
Loise KIm
Image: Instagram

Msanii Loise Kim kupitia kwenye ukurasa wake amewapa wanawake sababu ya kutowaacha waume zao endapo watawapata wametoka nje ya ndoa.

Pia aliwashauri wanawake wajue jinsi ya kukaa na waume zao na kukabiliana nao ipasavyo.

Mwanamuziki huyo alisema kwamba hajaweza kuhamazisha uzinzi wala mitala,lakini anasema ukweli kuhusu wanaume wengi.

 

"Mimi siyuko  hapa kuhamasisha uzinzi au mitala, lakini hapa ndipo tairi inagusa barabara. Katika ulimwengu huu niliko, nimejifunza kuwa,

..Hakuna mwanamke anayepaswa kumwacha mumewe kwa sababu amemuendea mwanamke mwingine, hakuna mwanamume aliye bora kuliko mwingine, ujue tu jinsi ya kumshughulikia na utatue maswala yako. 

Ikiwa utamwacha mumeo kwa sababu amechukua mwanamke mwingine na unafikiria kuwa utakwenda kupata mtu bora huko nje, samahani umekosea, mwingine ambaye ni mbaya kuliko mumeo.

Pigania mtu huyu ambaye ni wako. Kwa hivyo, wanawake, shikamaneni na wanaume wenu, jueni jinsi ya kushughulikia, suluhisha maswala yenu na ni jinsi gani mtambadilisha," Aliandika Loise.

Haya yanajiri baada ya drama baada ya drama kushuhudiwa , katika maisha ya ndoa ya watu mashuhuri huku wengi wakidaiwa wameenda nje ya ndoa.