Nilikuwa na mpenzi kwenye mitandao ya kijamii,hatujawahi kutana-Mwanamke asimulia

Muhtasari
  • Mwanamke asimulia jinsi alivyopatana na mpenzi mitandaoni
  • Kuna wale hupatana na wapenzi wao kwenye mitandao ya kijamii na kwa bahati nzuri wanafunga pingu za maisha
sad woman
sad woman

Ukidhani umeyasikia na kuyaona yote haya basi unayashuhudia mapya kila kuchao, je ni jambo lipi la kijinga ambalo ulifanya kwenye mitandao ya kijamii?

Kuna wale hupatana na wapenzi wao kwenye mitandao ya kijamii na kwa bahati nzuri wanafunga pingu za maisha.

Pia kuna wale ambao hupatana na watu kisha wanawatapeli kwa njia ya mapenzi.

Visa vya kutapeli kwenye mitandao ya kijamii vimekuwa vikivuma kila kuchao huku baadhi ya waliotapeliwa wakipata haki.

Mwanamke mmoja aliwaacha wengi wakiwa wamepigwa na butwaa baada ya kusimulia jinsi alipatana na mpenzi kwenye mitandao ya kijamii bali hawajawahi onana ana kwa ana.

"Mwaka wa 2017 nilipayana na mpenzi kwenye mitandao ya kijamii ya faceboo, akanitumia picha na nikamtumia zangu

Tulianza mahusiano ya kimapenzi, akaniambia niwe mpenzi wake na nikakubali, kwa maana mwanamke lazima awe na mahitaji nilikuwa nikimhitisha chochoe ananitumia pesa

Pia kuna wakai alinilipia karo ya chuo kikuu, lakini cha kushangaza nikimwambia tupatane alikuwa ananipa sababu nyingi ambazo haziishi

Sijui nilikuwa na chumbia illuminati au mtu wa kawaida, sijui kama picha ambao alikuwa ananitumia ni zake au ni za mu mwingine, sijui ni iiwete ama ni mtu wa aina gani

Ndio alinisaidia sana katika maisha yangu, natamani tu siku moja nimuone nimshukuru kwa yote ambayo alinitendea

Nilikosana naye nnikamwambia kama hataki tuonane haya basi mahusiano yetu yamekwisha," Alisimulia mwanamke huyo.