(+Video)Sijawahi lala na mtu kwenye tasnia ya burudani mpaka mahali nilipo-Msanii Zuchu adai

Muhtasari
  • Zuchu asema hajawahi lala na mwanamume yeyote kwenye tasnia ya burudani
  • Msanii huyo alifahamika sana baada ya kusajiliwa katika lebo ya WCB ambaye bosi wake ni staa wa bongo Diamond Platnumz
Zuchu-cover-for-her-new-song
Zuchu-cover-for-her-new-song

Msanii wa kike wa nyimbo za bongo kutoka Tanzania Zuchu akiwa kwenye mahojiano alisema kwamba hajawahi lala na mwanamume yeyote kwenye tasnia ya burudani.

Msanii huyo alifahamika sana baada ya kusajiliwa katika lebo ya WCB ambaye bosi wake ni staa wa bongo Diamond Platnumz.

Zuchu alianza kutoa kibao kimoja baada ya kingine huku akiwashirikisha wasanii wenzake katika baadhi ya nyimbo zake.

 

Msanii huyo alisema kwamba anaamini siku moja atafaulu katika kazi yake, huku akiwashauri wasanii wanawake kuwa yote yanaweekana katika tasnia ya burudani bila ya kulala na mwanamume yeyote katika tasnia hiyo.

Pia alisema kwamba hajawahi shikwa mkono na mwanamume yeyote bila idhini yake.

"Sijawahi lala na mtu yeyote katika music industry mpaka mahali nilipo,iwe mzalishaji, dj sijawahi mppaka mahali hapa nilipo

Ata kushikwa mkono sijawahi bila ruhusa yangu, kwa wasanii wa kike yote yanawezekana bila ya kulala na mwanamume ili muziki wako ujulikane." Alisema Zuchu.

Kibao chake cha awali kinachofahamika kama 'sukari'kimevuma sana kwenye mitandao ya kijaii na hata kupendwa na mashabiki.

Hii hapa video ya mahojiano hayo;