Wasanii wa kenya wanapaswa kuheshimiwa- Otile brown afichua haya

Muhtasari
  • Otile Brown asimulia changamoto wasanii wa kenya hupitia
  • Pia aliwakashifu watu ambao wanasema kwamba wasanii hawatilii bidii katika kazi yao
Otile Brown
Otile Brown

Msanii Otile brown kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alifichua changamoto ambazo wasanii wa humu nchini wanapitia.

Msanii huyo alisema si rahisi kwa msanii kufahamika wala kuendelea vyema nchini kenya.

Kupitia kwa ujumbe aliouandika kwenye ukurasa huo Otile alisema kwamba wasanii wa himu nchini wanapaswa kuheshimiwa.

 

"Nafikiria wasanii wa kenya wanapaswa kuheshimiwa...wasanii hao wote ambao huwa mnatulinganisha nao wana washauri wakubwa ambao waliwashika mkono, ata wakianguka tena watawashika mkono

Washauri wao pia wanawekeza pesa zao kwenye miradi yao, kukua kwetu lazima kukawie na kuwa kudogo kwa maana sisi huwa tunajianyia kila kitu wenyewe

Hatuna waekezaji,lebo nakumbuka hatujatoka kwa familia tajiri," Aliandika Otile.

Pia alizidi na kunakili ujumbe wke na kusema kuwa,

"Huwa tunagawanya mapato ndogo ambayo tunapata, kusaidia familia zetu, kulia deni zetu na pia kuwekeza katika biashara na kazi zetu za usanii

Tumeangushwa na serikali, tasnia ya burudani na pia  wadau  kwenye vyombo vya habari, kwa mfano wasambazaji wa miziki yetu ambao wanajinufaisha kutoka kwa wasanii 

Wengine watakuita mtulize tu na kunywa pombe na kukutambulisha kwa wanawake ili waonekane wao ndio kusema

 

Ndio maana nyinyi nyote hataweza kuniona karibu nao, kabla ya kuzungumza jua ya kwamba mnayoyaona na kufanya tunajifanyia sisi wenyewe

Na wale wanadhani wao ni bora kutushinda 'wamebebwa'kile tu wanafikiria ni jinsi ya kukua katika tasnia na katika muziki wao kwa maana kila kitu wamefanyiwa

Kwa upendo na kusema ukweli niko sawa na kukua kwangu, kwa hivyo wacheni kusema kwamba hatutii bidii katika kazi yetu," Alizungumza Otile.