'...Awe mfano kwa wasanii wengine,'Diamond ampongeza Rayvanny baada ya kuzindua lebo yake

Muhtasari
  • Msanii Diamond ampongeza Rayvanny kwa kuzindua lebo mpya ya muziki
Diamond Platnumz

Siku ya JUmanne msanii wa lebo ya WCB Rayvanny alizindua lebo yake ya muziki, huku hafla hiyo ikihudhuriwa na wasanii wenzake na marafiki.

Staa wa bongo Diamond alikuwa miononi mwa wasanii ambao walihudhuria uzinduzi wa lebo ya Rayvanny.

Huku akimpongeza alisema kwamba Rayvanny amekuwa mnyenyekevu na wala hakutumia dharau yeyote ili kuwa mkubwa au kwa umaarufu wowote.

 

Pia alisema kwamba Rayvanny anapaswa kuwa mfano mwema kwa wasanii wengine.

“Nimpongeze sana Rayvanny na awe mfano kwa wasanii wengine…maana wasanii wengine wanadhani kuwa ili uonekane mkubwa lazima utukane au udharau watu ambao ulikuwa unafanya nao shughuli…hakutaka kutumia ukubwa wake na pesa alizokuwa nazo kuwadharua watu. Alionyesha njia njema na ninaamini kuwa Mungu atampa baraka kubwa sana.

Inawezekana leo hii Rayvanny asema kuwa hela yake awekeze kwingine lakini ameona aanzishe Next Level Music ili awasaidie na vijana wengine," Alisema Diamond.

Rayvanny amekuwa katika lebo ya WCB kwa zaidi ya miaka 5, huku akizungumza alikuwa na haya ya kusema,

UNAIBIWA-BY-RAYVANNY-1-768x768
UNAIBIWA-BY-RAYVANNY-1-768x768

“Nina furaha kuona wote mmefika, niwashukuru viongozi wangu kwa kunisaidia kufikia hapa leo. Nina amini viongozi wangu wanafurahi kuona kijana wao anakuwa. Na pia nawaongeza heshima kuona kuwa pia nimefikia point ya kuwa daraja la kuwasaidia watu wengine. Pekee yangu singefika hapa lakininkwa mchango wao nimefika hapa leo,"

Miongoni mwa wasanii waliohudhuria hafla hiyo ni Baba Levo, Lil Ommy Queen Darleen, Dully Sykes, TID, Diamond Platnumz, Sallam SK, Babu Tale,Zuchu, Lava lava miongoni mwa wengine