(+Video) Sikutiwa mbaroni, nilikujiwa kuna tofauti ya kushikwa na kukujiwa-Erci Omondi aeleza

Muhtasari
  • Eric Omondi asema hakukamatwa bali alikujiwa
  • Eric alikamatwa kwa kukiuka sheria za filamu humu nchini, huku akiachilia Ijumaa, Machi 12 kwa dhamana ya shilingi elfu 50,000

Mchekeshaji Eric Omondi kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alieleza jinsi alikujiwa na maafisa wa polisi .

Huku akizungumza katika video aliopakia kwenye ukursa wakee w instagram mchekeshaji huyo alisma kwamba alikujiwwa bali hakukamatwa.

Eric alikamatwa kwa kukiuka sheria za filamu humu nchini, huku akiachilia Ijumaa, Machi 12 kwa dhamana ya shilingi elfu 50,000.

 

"Sasa kwa kuwa joto limewashuka… Naskia watu wanasema ati nilishikwa, mimi sikushikwa nilikujiwa kuna tofauti kati ya kushikwa na kukamatwa

… hivyo nimekaa kwenye roshani karibu saa tano asubuhi, ndipo naona kwa mbali magari manne na niko kama wale wanaenda wapi

alafu ndani ya dakika moja na nusu wamefika kwa kiwanja na wameingia kila mahali.

Jambo zuri ni kwamba walijitambulisha… na jambo bora kufanya ni kushirikiana kila wakati na serikali au polisi haswa wakati unajua hauna chochote cha kujificha

Ukiombwa simu peana. Wakachukua simu ya kila mtu. Shirikiana kila wakati na polisi kwa sababu inafanya mambo yawe rahisi kabisa," Aliongea Omndi.

Pia alifichua kwamba ilikuwa mara yake ya kwanza kukamatwa.

"Sijawahi kukamatwa, hiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza, sijui kwa sababu baba yangu alikuwa mkaguzi mkuu na OCS huko Kisumu, lakini dakika tatu za kwanza nilikuwa nimetetemeka

 

Lakini basi tena tulipoingia kwenye gari niliwachekesha, kutoka Barabara ya Kiambu mpaka Kituo Kikuu cha Polisi. Shirikiana kila wakati, serikali haina ubaya saa zingine,"