Onyesho la 'Wife Material' sio la familia Eric Omondi aweka wazi

Muhtasari
  • Kipindi cha mchekeshaji Eric Omondi cha 'Wife Material season 2' kinatarajiwa kurudi hivi karibuni baada ya kusimamishwa kwa muda
Eric Omondi

Kipindi cha mchekeshaji Eric Omondi cha 'Wife Material season 2' kinatarajiwa kurudi hivi karibuni baada ya kusimamishwa kwa muda.

Wasichana watakao kuwa kwenye kipindi hicho ni wa nchi tofauti, kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Eric amewaonya mashabiki kuwa sio kipindi cha familia yote.

Yaani sio kipindi ambacho ni cha kutazamwa na watoto wa shule .

 

Baada ya kipindi hicho kuanza wiki chache Eric alitiwa mbaroni kwa madai kwamba amekiuka sheria na kanuni za filamu nchini Kenya.

Eric amewaambia mashabiiki wake wajitayarishe kwa maana kipindi hicho kinarudi hivi karibuni.

"Kufikia sasa nadhani kila mtu anaelewa kuwa #WifeMaterial ni wazi sio onyesho la familia. Wote tumeelewa onyesho kwa sasa

Tunapojiandaa kurudisha # WifeMaterial2 ni muhimu kusema wazi kuwa onyesho hili ni PG . Tafadhali jiandae na uzingatie ipasavyoπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜ŠπŸ˜ŠπŸ˜ŠπŸ˜Š," Aliandika.