Wacheni kuwaambia watoto wenu baba zao walikanyagwa na lori-Msanii Loise Kim

Muhtasari
  • Msanii wa Kikuyu Loise Kim amewaacha mashabiki wake na gumzo kwenye mitandao ya kijamii ya instagram baada ya kuwaambiwa akina mama wawaonyeshe watoto wao baba zao
  • Msanii huyo akiwashauri akina mama alisema kwamba baraka nyingi hutoka kwa baba ya mtoto wa mtu
  • Huku akiandika ujumbe wake alilinganisha usemi wake na hadithi ya Rebecca kwenye biblia
Loise KIm
Image: Instagram

Msanii wa Kikuyu Loise Kim amewaacha mashabiki wake na gumzo kwenye mitandao ya kijamii ya instagram baada ya kuwaambiwa akina mama wawaonyeshe watoto wao baba zao.

Asilimia ya juu imeshuhudiwa nchini huku akina mama wanawalea watoto wao peke yao licha ya baba yao kuwa hai.

Kuna wale wanachagua kuwadanganya watoto wao kwamba baba yao alikufa, ilhali kuna wale huchagua kuwaonyesha baba wao.

Msanii huyo akiwashauri akina mama alisema kwamba baraka nyingi hutoka kwa baba ya mtoto wa mtu.

Huku akiandika ujumbe wake alilinganisha usemi wake na hadithi ya Rebecca kwenye biblia.

"Baraka hutoka kwa baba wa watoto; Ikiwa ni Mama, Rebecca angembariki mtoto wake. Wale ambao hawajaolewa na huwaambia Watoto wao kuwa baba yao alikanyangwa na lori; wacha tuungane na watoto wetu na baba zao na tutafute baraka hizi huko waliko🙏🏽." Aliandika Loise.

Ni ujumbe ambao uliibua mdahalo kati ya mashabiki, na haya hapa maoni ya mashabiki.

lucieshanmillan: And those rejected by their dads are not blessed in this case???

its_me_nytah: I believe blessings belong to God and Him alone

njugushjymo: Depends from case to case coz separations are different...I think the ultmost blessings comes from God...good day people.

kevohdancestar: Very true

princessmaggiekash2: Well stated, blessed day too

naomiwariara: Blessings comes from God,my ex husband tried to kill my son and I several times. Alafu nipeleke mtoto wangu huko eti ni blessings tunatafuta?Wacha Mungu anabarikie mtoto akipenda