'Kuwa na mpenzi sio jambo la muhimu kwa sasa,'Muigizaji Maria

Muhtasari
  • Muigizaji Maria aweka wazi hana mpenzi
  • Muigizaji huyo alisema kwamba baada ya kufahamika sana aliwapoteza marafiki wengi kwani walitaka mambo mengi kutoka kwake

Muigizaji Yasmin Saied anayefahamika sana kama Maria,kutok kwa kipindi kilichokuwa kinapeperushwa katika runinga ya Citizen 'Maria' akiwa kwenye mahojiano alisema kwamba kuwa na mpenzi si jambo muhimu kwake.

Maria alisema kwamba yeye  ni kijana na hamna haja ya kuharakisha kupenda, licha ya hayo yeye ni wa dini ya kiislamu na kuchumbiana si jambo nzuri kulingana na dini yao.

Pia aliweka wazi kuwa kuwa na mchumba kutampelekea kufanya mambo ambayo hayastahili, na licha ya hayo ni vyema kupenda na kuwa na mpenzi.

 
 

Alisema kwamba alikuwa na mpango wa kujiunga na cuo kikuu mwaka jana 2020, lakini corona ikaharibu killa kitu.

Muigizaji huyo alisema kwamba baada ya kufahamika sana aliwapoteza marafiki wengi kwani walitaka mambo mengi kutoka kwake.

Maria alisema kwamba mama yake ndiye meneja wake.

"Mimi pia ni muslim na kuchumbiana katika dini yetu ni haram,jambo la muhimu na lininalo faa ni kungoja mume wako wa ndoa

Kuwa na mpenzi inaweza fanya ufanye mambo mengi,ni vyema kuwa na mpenzi kwa maana utafurahi lakini lakini huwezi fahamu matokeo yake

Kuwa na mpenzi si jambo la muhimu kwa sasa au sijaweza kuweka kama jambo muhimu," Maria Aliongea.