Usimuamini mtu ambaye anachukua muda mwingi kujibu ujumbe wako-Ushauri wake Samidoh

Muhtasari
  • Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram msanii huyo amekuwa akiwashauri mashabiki wake kwa jambo moja au nyingine
samidoh 3
samidoh 3

Msanii Samuel Muchoki almaarufu Samidoh anafahamika kama mkuu wa nyimbo za kikuyu, kwa sababu nyimbo zake zinapendwa sana na mashabiki wake.

Miezi chache iliyopita Samidoh alivuma sana kwenye mitandao ya kijamii baada ya mama wa mtoto wake mwanasiasa Karen Nyamu kufichua kwamba yeye ni baba wa mtoto wake.

Ni jambo na habari ambazo zilimfanya Samidoh aombe msamaha kwa familia yake hasa mkewe na mashabiki wake.

 

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram msanii huyo amekuwa akiwashauri mashabiki wake kwa jambo moja au nyingine.

Siku ya Jumatano msanii huyo aliwashauri mashabiki wake wasimuamini mtu yeyote ambaye anachuku muda mrefu kujibu jumbe zao.

Huu hapa ujumbe wake;

"Usiwahi muamini mtu ambaye anachuku muda mreu kujibu ujumbe wako, lakini wakati wako na wewe kila wakati wamo kwenye simu zao," Aliandika Samidoh.