Mfunge mume wako nyumbani kama hutaki ahusike na wanawake wengine-Akothee

Muhtasari
  • Msanii Akothee awaambia wanawake ambao wako kwa ndoa haya
  • KUpitia kwenye ukurasa wake wa instagram Akothee alipakia video huku akiwashauri wanawake waache kulalamika kuhusu waume wao kila wakati

Msanii Esther Akoth almaarufu Akothee alionekana kugadhabishwa na tabia za baadhi ya wanawake ambao wamo katika ndoa.

KUpitia kwenye ukurasa wake wa instagram Akothee alipakia video huku akiwashauri wanawake waache kulalamika kuhusu waume wao kila wakati.

Pia msanii huyo aliwashauri wanawake hao kama hawataki wanaume wao wapende wanawake wengine basi wanapaswa kuwafunga nyumbani badala ya kulalamika.

 

"Achana na mwanamume wangu, mwanamume yupi huyu unaongelelea ambaye ulimzaa, mwenye hutaki wanawake ambao hawana waume na wapenzi wajifurahishe na yeye kidogo

ulikuwa na naye wakati wote  wa corona, kwani huwezi saidiwa usije hapa na kuanza kutuambia tuachana na mume wako

wanawake wote ambao wameolewa, kama hutaki kushiriki mume wako na wanawake wengine basi mfunge kwa nyumba

Na usikuje hapa kusumbua akili zetu, ukituambia tuachane na mume wako," Akothee alisema.

Hii hapa video ya msanii huyo akisema hayo;