Sonko amwandikia mwanawe ujumbe maalum siku yake ya kuzaliwa

Muhtasari
  • Sonko amwandikia mwanawe ujumbe maalum siku yake ya kuzaliwa
  • Gavana wa zamani wa kaunti ya Nairobi MIke Sonko ana wasichana wawili ambao wanafahamika sana kwenye mitandao ya kijamii
Sandra Sonko
Image: Facebook

Gavana wa zamani wa kaunti ya Nairobi MIke Sonko ana wasichana wawili ambao wanafahamika sana kwenye mitandao ya kijamii.

Saumu Mbuvi na Sandra Mbuvi,Sandra sku ya Ijumaa tarehe 2 Aprili amesheherekea siku yake ya kuzaliwa kwa njia ya kipekee.

Huku ikiwa ni siku yake ya kuzaliwa sio ajabu kumuona Mike aimwandikia wala kumfanyia jambo la kipekee.

 

Kupitia kwenye ukurasa wake wa facebook Sonko alimwamndikia Sandra ujumbe wa kipekee huku akimlimbikizia sifa.

Sonko alimwambia mwanawe kuwa huwa anamshangaza kila kuchao, na amekuwa mtu wa kujali.

"Kwa binti yangu mpendwa Sandra: Kwa kila siku ya kuzaliwa inayopita, unanishangaza zaidi na zaidi

Umekua mtu mwenye akili, wa kufurahisha na anayejali ambaye anaendelea sana  maishani mwake. Nimefurahi kuona nini siku zijazo zimekuwekea. Heri ya kuzaliwa binti yangu kipenzi, nakupenda siku zote.," Aliandika Sonko.

Awali Sonko amekuwa akipitia changamoto nyingi.