Sijafungiwa nyumba,nilionyesha kile watu wanapitia wakati huu,'Akuku Danger aweka mambo wazi

Muhtasari
  • Mchekeshaji Akuku Danger aweka wazi hajafungiwa nyumba
  • Pia aliweka wazi kwamba baada ya video yake kuenea sana aliweza kupokea msaada kutoka kwa wasamaria wema ambao walimtumia pesa
akukua2
akukua2

Tarehe 1, Aprili mcekeshaji wa kipindi cha Churchill Mannerson Oduor Ochieng  almaarufu Akuku Danger alipakia video iliyoonyesha akifukuzwa kwa nyumba kwa sababu ya kutolipa kodi.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram hatimaye amezungumzia tukio hilo huku akisema kwamba ni jambo ambalo wakenya wengi wanapitia hasa wakati huu wa janga la corona.

Pia aliweka wazi kwamba baada ya video yake kuenea sana aliweza kupokea msaada kutoka kwa wasamaria wema ambao walimtumia pesa.

"Nimeona mambo yangu yakiwa yamesemwa baada yangu kupakia video nikifukuzwa kwa nyumba kwa ajili ya kutolipa kodi

Mengi yalisemwa kwamba Akukudanger hana nyumba,wakati mwingine unafika unataka kuburudisha mtu na kufunza, wakati huo nilikuwa nataka kufunza

Ni jambo ambalo halikunitendekea lakini limetendekea mtu unamjua, inaweza kuwa rafiki yako,binamu yako,ndugu yako au binamu yako

Sababu ya kufanya video hiyo ilikuwa ya kumpa Uhuru ujumbe afungue nchi etu kwa maana watu wengi wamepoteza kazi," Alisema Akuku Danger.

Mchekeshaji huyo alisema kwamba pesa ambazo alipokea kutoka kwa wasamaria wema ata wasaidia wakenya ambao wana shida tofauti na hawajiwezi.

Hii hapa video ya mchekeshaji akieleza, sababu ya video hiyo;