'Mtakuja kanisani tena kuomba kura.' Mhubiri Ng'ang'a akashifu serikali kwa kufunga makanisa

Muhtasari
  • Muhubiri Ng'ang'a akashifu serikali kwa kufunga makanisa
  • Pia aliguzia jinsi wanasiasa walianza kufanya kampeni za siasa na kusambaza corona
  • Wimbi la tatu la maambukizi ya virusi vya covid-19 lilipelekea Rais Uhuru Kenyatta kufunga kaunti tano zilizokuwa zimeathirika sana
Mzqk9kpTURBXy81NDQ2MGRiMTk1ZTMwNGE2OTc1NDgzZTdkYjFhNDk3Ny5qcGeSlQMADc0Cr80BgpMFzQMUzQG8gaEwAQ
Mzqk9kpTURBXy81NDQ2MGRiMTk1ZTMwNGE2OTc1NDgzZTdkYjFhNDk3Ny5qcGeSlQMADc0Cr80BgpMFzQMUzQG8gaEwAQ

Muhubiri  James Ng'ang'a amewakashifu wanasiasa kwa  kutozingatia masharti ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona yaliowekwa na wizara ya afya.

Kupitia kwenye video iliyopakiwa kwenye mitandao ya kijamii ya youtube Ng'ang'a alisema kwamba anazungumza kama mkenya ambaye anahitaji haki yake.

Pia aliguzia jinsi wanasiasa walianza kufanya kampeni za siasa na kusambaza corona hata baada ya rais Uhuru Kenaytta kupiga marufuku ya mikutano ya siasa.

 

Nga'ng'a alisema baada ya serikali kusababisha kusambaa kwa virusi hivyo alisema kwamba kanisa ndilo linapewa adhabu licha yao kutosababisha msambao wa virusi hivyo.

"Nyinyi ndio Mlisambaza hii kitu, mlisema iko na kweli iko. Sisi Hatuendangi Crusade, mlitufungia Crusade, ninaongea kama mtume na mkenya ambaye ako na haki ya kuongea.

Sisi hatukuenda Crusade Kanisani, mimi niko na Lorry iko hapa nje, hatukuenda Crusade, tukatii hiyo. Nyinyi wenyewe mkaanza BBI, Chama hiki, chama hiki.

Ikifika ni kanisa Corona inaanza. Sasa BBI imepita kanisa ndo iko na shida. Unless nyinyi wenye mnapigana na watu wasikuje kanisa sababu nyinyi wenyewe mtakuja tena kanisa kuomba kura huko.

Naitwa James Maina Ng’ang’a nilitairiwa 1972, na nilizaliwa 1953 liwalo na liwe. Yesu anaokoa na anaponya, kama hatakuponya mimi ameniponya na ameniokoa. Nitamsifu, hata kama nitakufa na Corona ama nini , sina shida hiyo. Shida yangu ni leo.

Polisi kuingia kwa kanisa na kupiga watu watatu, na jana mazishi imezikwa mheshimiwa Koinange na amepewa TV Live na kanisa watu watu wanapigwa," Nga'ang'a alisema.

Wimbi la tatu la maambukizi ya virusi vya covid-19 lilipelekea Rais Uhuru Kenyatta kufunga kaunti tano zilizokuwa zimeathirika sana.

Kaunti hizo ni pamoja na  Nairobi, Nakuru, Kiambu ,Kajiado na Machakos.

Hii hapa video akizungumza;

Angry Pastor James Ng’ang’a lectures the government over closure of Churches/Pastor Ng'ang'a