Wanaume mnapaswa kuacha kufanya haya kama mnataka wanawake warembo

Muhtasari
  • Wanaume mnapaswa kuacha kufanya haya kama mnataka wanawake warembo
  • KIla mwanamume huwa anajivunia wakati anatembea na mpenzi wake huku akisifiwa kwa urembo
sad man
sad man

KIla mwanamume huwa anajivunia wakati anatembea na mpenzi wake huku akisifiwa kwa urembo.

Mwanamke mrembo sio urembo tu kwa sura bali jinsi anavyo tumia akili na kuchukulia mambo na changamoto katika uhusiano wao wa kimapenzi.

Katika makala haya tutazingatia mambo ambayo wanaume wanapaswa kuacha kufanya karne hii ya sasa ili ampate mwanamke mrembo.

 

1.Wacha ufeki maisha

Wanaume wengi humu nje wanafeki maisha yao ili kuwapendeza wanawake bila ya kujua wanachotaka maishani mwao.

Uhusiano kama huo haudumu kamwe bali utapata wawili hao wanakorofishana kila kuchao.

2.Usiende kila mahali mpenzi wako yuko

Utapata wanaume wengi wanwachunga wanwake wao na kufuatilia maisha yao,jambo hilo hufanya mwanamke kufikiria kwamba anafuatwa kila mahali aendapo.

3. Acha kuwa mkali sana

KUna baadhi ya wanaume ambao ni wakali sana kwa wapenzi wao, wanaume ukiwa mkali kwa mpenzi wako kwa kweli atakuogopa, na kuhisi kwamba hataki kuwa katika uhusiano huo tena.