Nitafute mpango wa kando?mume wangu ni mlevi chakari-Mwanamke asimulia

Muhtasari
  • Mwanamke asema kwamba anataka mpango wa kando baada a muewe kusahau majukumu yake
black-woman-crying-
black-woman-crying-

Maisha ya ndoa ni maisha ambayo watu au mtu uamua kwa moyo wake, na kuwa tayari kupambana na changamoto zozote katika maisha.

Kuna baadhi ya watu ambao wamepitia changamoto nyingi huku wakikata tamaa na kujutia kwanini waliinia katika ndoa.

Mama mmoja waliwaaacha mahabiki wa radiojambo mdomo wazi baada ya kusimulia jinsi mume wake amesahau na majukumu yake.

Kisa cha kusahau na majukumu yake ni kwamba amekuwa mlevi kupindukia.

"NImekuwa  wa ndoa kwa miaka mitano, mimi na mume wangu tumebarikiwa na watoto watatu, mume wangu alianza kubugia vileo miaka mitatau iliyopita

Amesahau ,ajukumu yake kama mume na baba wa watoto wangu hata mshahara wake anatumia kwa kubugia vileo

Nimechoka na maisha yake, kwa maana amesahau majukumu yake, nasikia nimechoka kabisa sijui ama nitafute mpango wa kando atimize mahitaji yangu," Alisimulia mwanamke huyo akilia.

Ni ushauri upi ambao unaweza kumpa mwanamke huyo?