Usipate watoto na mtu ambaye hauna uhakika naye-Anerlisa awashauri wanawake

Muhtasari
  • Anerlisa Muiai kupitia kwenye mitandao yake ya instagram amewashauri wasichana na wanawake dhidi ya kupata watoto na mtu ambaye hawana uhakika naye

Anerlisa Muiai kupitia kwenye mitandao yake ya instagram amewashauri wasichana na wanawake dhidi ya kupata watoto na mtu ambaye hawana uhakika naye.

Kulingana na Anerlisa ni sawa kuwa mpenzi wa mtu na hata kuvishwa pete ya uchumba lakii hamna mtu anapaswa kulazimshwa kupata mtoto kama hayuko tayari.

"Ni heri mpenzi wako akuache kwa ajili huna uhakika unataka kupata mtoto naye kuliko kulazimishwa

 

Wapenzi wasicha wadogo, usipate watoto na mtu ambaya huna uhakika naye, mnaweza chumbiana, kupendana na kadhalika lakini watoto?

Hayo yote ni kujitolea, hayo ni maoni yangu wengine wana maoni yao," Alisema Anerlisa.

Usemi wake unajiri siku chache baada ya kuwaonya wanaume ambao wamekuwa wakimtumia jumbe ili awe mpenzi wao.

Anerlisa alisema kwamba ukiweza ona DM wake utadhani kwamba alikuwa na ushindani wa kumtafuta bwana.