'Wacheni kunitumia picha mkiwa uchi ni sura mbaya,'Akothee awaonya wanaume

Muhtasari
  • Akothee awaonya wanaume wenye tabia ya kumtumia picha wakiwa uchi
akoth
akoth

Kwenye mitandao ya kijamii utapatana na watu wenye tabia mbaya na wenye hawana aibu, ambao watakutumia picha wakiwa uchi na kutaka uwe mpenzi wao.

Msanii Akothee amewaonya wanaume wa aina hiyo ambao wamekuwa wakimtumia picha wakiwa uchi.

KUlingana na msanii huyo picha hizo ni sura mbaya na amekuwa na taabu sana kuingia kwenye DM yake kwa ajili ya picha hizo.

 

"Tafadhali watu wacheni kunitumia hizo viungo vibaya, ni jambo lisilo na heshima kutuma picha kama hizo, sijawahi jua kama wanaume wanaeza tuma picha kama hizo

Naogopa ata kuingia kwenye DM yangu kwa ajili ya picha hizo nisipatane nazo," Aliandika Akothee.

Je umewahi patana na watu kama hao, kwenye mitandao yako ya kijamii?