'Kama mzazi unaweza kubali mtoto wako aolewe kwa ajili ya pesa?'Mike Sonko auliza

Muhtasari
  • Gavana wa zamani wa kaunti ya Nairobi Mike Sonko amewashauri wanandia na wapenzi jinsi ya kutatu shida katika uhusiano na ndoa zao
Gavana wa zamani wa Nairobi Mike Sonko

Gavana wa zamani wa kaunti ya Nairobi Mike Sonko amewashauri wanandia na wapenzi jinsi ya kutatu shida katika uhusiano na ndoa zao.

Miezi chache iliyopita tumeshuhudiwa wapenzi na wanandoa wakitoana uhai kwa ajili ya matatizo yao kwenye ndoa.

Sonko aliwashauri  wanandoa kwamba wanapaswa kuheshimu wapenzi wao na wazazi wao.

Pia mwanasiasa huyo alipakia video kwenye ukurasa wake wa facebook, na kuwauliza mashabiki na wazazi kama wanaweza kubali wasicha wao waolewe kwa ajili ya pesa.

Usemi wake Sonko unajiri siku chache baada ya kinara wa ODM Raila Odinga, kukashifu visa vya mauaji ambavyo vinaendelea kuripotiwa kila kuchao.

"Hii mambo ni kujipanga mapema. Lakini pia tuheshimu wazazi wetu, mabibi zetu, na watoto wetu

Kesi za hivi majuzi za unyanyasaji wa nyumbani zinazohusu mauaji ya wenzi wa ndoa, watoto na hata wazazi kama kisa cha kijana huyo huko Kisumu zinasumbua sana, na tunahitaji kumaliza utamaduni huu mbaya kama Wakenya. Siri pekee ya kuishi kwa ndoa yoyote au uhusiano, wakati mke wako juu wewe kuwa chini and vice versa. Ukikosa Sema pole and vice versa. Hasira hasara."

Baada ya kupakia video hio Sonko aliuliza swali hili;

"Sisemi kitu lakini ndoa kama hii itadumu, kama mzazi utamkubali msichana wako aolewe kwa ajili ya pesa,"