Tukipatana usiniulize kile huwa napakia kwenye mitandao ya kijamii-Akothee awaonya mashabiki

Muhtasari
  • Ni nani hamfahamu msanii Esther Akoth almaarufu Akothee, ni mwanamuziki na mama wa watoto 5 ambao huwa anajivunia kuitwa mama

Ni nani hamfahamu msanii Esther Akoth almaarufu Akothee, ni mwanamuziki na mama wa watoto 5 ambao huwa anajivunia kuitwa mama.

Akothee anafahamika sana kupitia kwa nyimbo zake tofauti na zile amefanya collabo na wasanii tofauti.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram msanii huyo amewaonya mashabiki wake dhidi ya kumuuliza kile huwa anapakia kwenye mitandao ya kijamii wakipatana ana kwa ana.

Huku akiwaonya mashabiki wake amewapa tahadhari endapo watamuuliza swali hilo atampa block wenye mitandao ya kijamii au kumlenga milele.

Alisisitiza kwamba hamna mtu ambaye anafahamu mitadao ya ijamii kama anavyoifahamu.

"Kama unataka kuwa ukizungumza na mimi usiniulize kila huwa napakia kwenye mitandao ya kijamii

Hautaelewa chochote na sitaweza kukueleza kitu chochote, tukipatana ana kwa ana usilete ujinga wa mitandao ya kijamii

Nitakuacha, nikupe blocj au nikulenge milele," Aliandika Akothee.