'...Tulikuwa na matumaini makubwa,'Msanii Emmy Kosgei aomboleza vifo vya rafiki zake

Muhtasari
  • Msanii wa nyimbo za injili Emmy Kosgei ametangaza vifo vya rafiki zake kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram 

Msanii wa nyimbo za injili Emmy Kosgei ametangaza vifo vya rafiki zake kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram huku akisema kwamba hajaamini kuwa wawili hao wameaga dunia.

Huku akiwaomboleza alianddika ujumbe huku akifichua jinsi walivyokuwa wamezungumza nao na kuwa na matumaini makubwa kwamba watatoboa.

"Nimehuzunishwa tu tangu nilipopata habari kuwa hamyupo tena! tuliongea na kuomba siku chache zilizopita tulikuwa na matumaini makubwa na tukijaa imani kwamba mtatoboa ... 😪😔 mlikuwa wa pekee sana kwangu na watu wengine wengi .. asante kwa kunishika mkono ..." Aliandika Emmy.

Msanii huyo hakufihua kiini cha kifo cha marafiki zake,bali alifichua kwamba walikuwa wanapitia magumu na changamoto katika maisha yao.

Pia alituma risala za rambi rambi kwa familia za wawili hao.

"kwa kunishangilia! Wewe na dada zako wa ajabu ni wanadamu wa kushangaza ... dua zangu na salamu za pole kwa mheshimiwa@sarahtunai #saima na wewe familia nzima, Boits na Mabinti wenzangu wa Baringo #DOB 😭 mutyo kukosa ..

pumzika kwa nguvu senge wangu mpendwa @ famboit umeenda kujiunga na # kupumzika kwa kifua cha bwana wetu. tunaishi kwa ukali kwa wakati wa kukopa!,"