'Nilikuwa nikipinga ndoa zamani,'Vera Sidika afichua siri ya jinsi ya kuwa kwenye ndoa

Muhtasari
  • Vera Sidika afichua siri ya jinsi ya kuwa kwenye ndoa
  • Mwanabiashara huyo alifichua kwamba hapo amani alikuwa anapinga ndoa kwani hakuwa anaamini maisha ya ndoa
Vera-and-Brown-Mauzo-696x418
Vera-and-Brown-Mauzo-696x418

Mwanasosholaiti Vera Sidika na msanii Brown Mauzo wamekuwa pamoja kwa zaidi ya mwaka mmoja, huku baadhi ya mashabiki wakidai kwamba hawayuko kwenye ndoa bali huo wao ni mchezo wa kuigiza.

Ni madai ambayo Vera alifutilia mbali kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram.

Mwanabiashara huyo alifichua kwamba hapo amani alikuwa anapinga ndoa kwani hakuwa anaamini maisha ya ndoa.

 

Huku akimjibu mmoja wa mashabiki wake aliyemuuliza jinsi maisha ya ndoa yako, alikuwa na haya ya kumwambia;

"Kusema kweli ni maisha mazuri,sijawahi fikiria kwamba yatakuwa mazuri,nilikuwa napinga ndoa zamani lakini nafikiria unapaswa kuwa kwa ndoa na mtu anayefaa," Alisema Vera.

Vera alifunga pingu za maisha mwaka jana katika harusi ya faragha,pia alisema kwamba amefika mahali ya ndoto yake kwa maana ana familia, afya njema na hata mume ambaye anampenda.