Muigizaji wa kipindi cha Pete Gillie Owino aaga dunia

Muhtasari
  • Muigizaji Jasiri aomboleza kifo chake mzee Msiri

Muigizaji wa kipindi cha 'Pete kinachopeperushwa katika runinga ya Maisha Magic Est Gillie Owino almaarufu mzee Msiri ameaga dunia.

Ni muigizaji ambaye aliigiza kama mzee wa kijiji cha funzi, na ambaye alikuwa na mawaidha mema.

Kifo chake kilitangazwa na runinga hiyo huku baadhi ya waigizaji wakituma risala za rambi rambi.

 

Muigizaji Mutrah Tamim maarufu Jasiri kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alituma ujumbe wake wa rambi rambi na kusema kwamba ni jambo ambalo hawakuwa wamelitarajia.

Huu hapa ujumbe wake;

"Hatuyuko tayari kusema kwaheri milele,ata kama tunajua na kufahamu kuwa ni hali ya maisha mioyo yetu ina uzito kwa kumpoteza mtu wa kipekee

Lakini tunapo kuomboleza pia tunasheherekea maisha yako, lala salama mzee msiri," Aliandika Jasiri.

Sababu ya kifo chake haijabainika, wala kutangazwa, hizi hapa baadhi ya jumbe za mashabiki;

wizkhaleenho: Pole sana broπŸ’”πŸ’”πŸ’”πŸ’”πŸ˜”

amfahima: Innalillah wainna illah rajuin. 😒so sad jamani

 

shekhaakida: Dah RIP mzee msiri

kim_kendrah: RIP Mzee msiri 😭😭😭

fnestry: So sad mzee msiri jaman 😒😭😭

furaha_alfredy_: Pumzika kwa Amani mzee msiri

tmkambi: Innalillah Wainna Illah rajiun Allah amjaalie pepo ya daraja la juu kabisa Aamiin 😭

lizy_eliza_beth_luoga: Mzee msiri....jamanii umetuacha

Kutoka kwetu wanajambo Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.