Sauti ya wanyonge au kuanguka?Sababu askofu Migwi kujiunga na siasa ni mwanzo wa kuanguka kwake

Muhtasari
  • Askofu Godgrey Migwi amepanga kujiunga na siasa katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022, na kuwania kiti cha ubunge cha wadi ya Mathioya
  • Je Migwi atakuwa sauti ya wanyonge au anatafuta jinsi ataanguka hasa katika kueneza neno lake Mungu

Askofu Godgrey Migwi amepanga kujiunga na siasa katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022, na kuwania kiti cha ubunge cha wadi ya Mathioya.

Kulingana na bango lake la siasa askofu huyo yuko tayari kunyakua kiti hicho.

Lakini tumewaona wengi wa watumishi wake Mungu wakijiunga na siasa na kisha kufifia kila kuchao, ama hawakukosea waliposema kwamba siasa mchezo mbaya.

Je Migwi atakuwa sauti ya wanyonge au anatafuta jinsi ataanguka hasa katika kueneza neno lake Mungu.

Hizi hapa sababu ambazo zinathibitisha kwamba Migwi akijiunga na siasa ndio mwanzo wa kuanguka kwake.

1.Muda

Migwi hatakuwa na muda wa kuhubiri neno lake Mungu kwani atatumia muda wake mwingi kujipigia debe, na kama atakuwa mbunge atakuwa akitimiza matakwa ya wananchi.

2.Matamshi

Kama mtumishi wake Mungu unahitajika kuwa na matamshi mema lakini tunafahamu vyema kwamba wanasiasa wengi hutumia maneno machafu.

3.Umakini

 

Askofu huyo hatakuwa na umakini mwingi katika neno la bwana bali atakuwa ameshikana na siasa na kuachia watu wengine majukumu yake.

Biblia inasema kwamba kama wataka kuwa karibu na MUngu lazima uombe na kusoma neno lake.

KUlingana na maoni yako ni vyema askofu huyo kujiunga na siasa licha yake kuwa mtumishi wa Mungu, na licha ya kuona wengi ambao walijiunga na siasa lakini hatuwasikii wakati huu wala kuwaona.