DNA yaonyesha Kabi Wajesus ni babaye mtoto wa binamu yake,athibitisha habari hizo

Muhtasari
  • DNA yaonyesha Kabi Wajesus ni babaye mtoto wa binamu yake,athibitisha habari hizo
Kabi wa jesus
Kabi wa jesus

Kabi Wajesus kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amekiri kwamba ni baba yake Abby ambaye mama yake anafahamika kama Shiko.

Awali kupitia kwenye youtube Kabi alidai kwamba mwanamke huyo anayedai kwamba ana mtoto naye ni binamu yake.

Baada ya DNA kufanywa matokeo yalionyesha kwamba Kabi ni baba wa mtoto huyo, ambapo alisema kwamba kitendo hicho kilitendeka wakati hakuwa ameokoka.

 

Aliwaomba mashabiki wake msamaha hukku akisema kwamba atajukumikia mahitaji ya mwanawe.

"Haya Jamaa na msifu Yesu,Baadhi yenu mnaweza kujua kuhusu jambo linalohusu mimi kuhusu mtoto Abby.

Ninataka kudhibitisha kuwa Jana matokeo ya baba yalitolewa ambayo yalithibitisha kuwa mimi ndiye baba mzazi wa mtoto. Matokeo yanathibitisha kuwa, mnamo 2013 (ambayo ilikuwa kabla ya kuokoka na kuoa), 

Najua habari hii inashtua wengi wenu ambao mnafuata na kututazama. Ninajua pia kuwa maoni yangu ya umma juu ya jambo hili yalitoa maoni ya uwongo ambayo najuta sana.

Sasa kwa matokeo ya baba yatoka, ni raha kwani tunaweza sasa kuzungumza mbele na mama kwa ustawi wa mtoto wetu. Mara moja namfikia ili tuweze kujadili na kukubaliana juu ya maisha yake ya baadaye.

Kama sisi sote tunakubaliana na ninakubali, masilahi ya mtoto ni muhimu zaidi.

Najua ni lazima nichukue jukumu kamili kwa matendo yangu yote, kwa mtoto wangu, kwa familia yangu na pia kwa mashabiki wangu. Nimeomba msamaha kutoka kwa Mungu, familia yangu na pia ninaomba msamaha kwa mashabiki

 

Kusonga mbele nitafanya kila kitu katika uwezo wangu kumtunza mtoto wangu, kama baba," Aliandika Kabi.

Miezi mitatu iliyopita Kabi alikana madai wamba ni baba yake Abby, huku akisisitiza kwamba Shiko ni binamu yake na wala sio mama wa mtoto Abby.