'Staki watoto wengine!' Tugi awaambia Njugush na Wakavinye

Njugush-son-Tugi-696x418
Njugush-son-Tugi-696x418

Kila uchao, Blessed Tugi ambaye ni mwanao mcheshi Njugush na Celestine Ndinda, anazidi kutupa sababu ya kutabasamu kwa ajili ya vituko vyake.

Licha ya umri wake mchanga, Tugi ana uwezo wa kuumiza mbavu za wachanga na wazee kwani ni dhahiri ana talanta ya ucheshi kama babake Njugush.

Hii leo ikiwa siku ya kusherehekea kina mama wote duniani, Njugush alimuandikia mkewe, ujumbe wa kumsifu kwa kumpa kijana mtanashati.

Alimalizia ujumbe akisema kuwa anatumai kuwa atampa watoto wengi zaidi.

Hapo awali, Njugush alikuwa amechapisha video aliyomrekodi Tugi akisema kuwa hataki mtoto mwingine katika familia yao na kuwa yeye pekee yake ametosha.

Tugi anaskika akisema; ah ah sitaki watoto wengine mimi nimetosha!

Tazama kanda ifuatayo