'Asante kwa kunisikiza,'Bahati amshukuru Diamond baada ya kupatana Afrika Kusini

Muhtasari
  • Bahati amshukuru Diamond baada ya kupatana Afrika Kusini

Msanii Bahati amemshukuru staa wa bongo Diamond Platnumz kwa kuwa naye katika safari yake ya usanii na kumpa ushauri iwezekanavyo.

Msanii huyo aliandika hayo kwenye ukurasa wake wa instagram baada ya wawili kupatana Afrika Kusini ambapo Diamond amekuwa kwa wiki chache.

Bahati alifichua kwamba anatoa albamu yake mpya hivi karibu na anatumai kwamba itakuwa bora zaidi.

 

"Jana Usiku huko Joburg Afrika Kusini Nikiwa na Mwanamuziki Nambari # 1 Afrika @DiamondPlatnumz 🌍 ndugu yangu Asante kwa kunipa sikio na mwongozo kila wakati; Sijawahi Kuchukua kwa mzaha

Maneno na Ushauri Wako JanaπŸ™Œ Najua Hiyo Itafanya Albamu Yangu Ijayo Kuwa Moja  Bora Niliyowahi Kufanya! Ninanyenyekea πŸ™ Asante kwa Kuwa Daima Ndugu Mkubwa zaidi," Aliandika Bahati.

Bahati amekuwa akitia bidii katika kazi yake ya usanii huku akitoa vibao kadha wa kadha huku akiwashirikisha wasanii tofauti.