Awali nimeulizwa na wanaume wenye pesa niwazalie watoto nikakataa-Vera Sidika

Muhtasari
  • Wengi wakimtazama mwanasosholaiti Vera Sidika  watasema kwamba ni mwanamke ambaye anapenda pesa, lakini kwa kweli ni mwanamke ambaye anatia bidii katika kazi yake
Vera-and-Brown-Mauzo-696x418
Vera-and-Brown-Mauzo-696x418

Wengi wakimtazama mwanasosholaiti Vera Sidika  watasema kwamba ni mwanamke ambaye anapenda pesa, lakini kwa kweli ni mwanamke ambaye anatia bidii katika kazi yake.

Kupitia kwenye mirandao ya kijamii ya instagram Vera alifichua kwamba kuna baadhi ya wanaume ambao walikuwa wanamsihi awazalie watoto na kumchumbia bali licha ya wanaume hao kuwa na pesa aliwakataa.

"Nilichagua upendo maishani mwangu, kutoka kitambo sijawahi kuwa mwanamke ambaye anatamani kuolewa na mwanamume mwenye mali nyingi au Milionea au bilionea

Halijakuwa jambo ambalo ni la kutamani,awali nimechubiwa na hata kuulizwa na wanaume wenye pesa ni wazalie watoto lakini nilikataa," Alisema Vera.

Mwanasosholaiti huyo alifichua kwamba rafiki zake walikuwa wanaona kwamba hayuko makini na maisha yake kwa kukataa mahitaji ya wanaume hao.

"Baadhi ya marafiki zangu wakati huo walifikiria kwamba nina wendawazimu,sijawahi kuwa mwanamke amabye anatahitaji mtoto wa tajiri yaani 'ATM Baby'

Huwa nawaita hivyo kwa maana wanawake wengi wanataka kuwa na watoto na wanaume tajiri ili wapate pesa kutoka kwao

KIla wakati wanapomuona mtoto huyo washaafanya heshabu ya jinsi ya kupiga simu, na kuuliza pesa

Sijawahi kuwa mwanamke wa haina hiyo, nilitaka kupata mtoto kutoka kwa upendo," Alisema.

Vera kwa sasa ni mkewe Brown Mauzo, je wanwake wanapaswa kuacha tabia ya kuwatumia watoto wao kuitisha wanaume pesa?