'Aidha wewe ni wangu au la,' Tanasha Donna ataja anayotarajia kutoka kwa mumewe wa maisha

Muhtasari
  • Baada ya Tanasha Donna kuachana na staa wa bongo Diamond Platnumz, hajaweza kumpata mpezni mwingine bali amekuwa akita bidii katika kazi yake ya usanii
Tanasha
Tanasha Donna Tanasha

Baada ya Tanasha Donna kuachana na staa wa bongo Diamond Platnumz, hajaweza kumpata mpezni mwingine bali amekuwa akita bidii katika kazi yake ya usanii.

Tanasha na Diamond waliachana mapema mwaka wa 2020, huku ikimlazimu Tanasha kurudi Kenya na mwanawe.

Kupitia kwenye mitandao ya kijamii ya instagram msanii huyo ameweka matarajio yake kwa atakaye kuwa mumewe wa maisha.

 

"Mpenzi mume wangu wa maisha tunaweza jenga haya pamoja lakini weka haya kwa akili, huwa sichezi michezo aidha wewe ni wangu au la

Kama mwanamke anakutania ni afadhali umwambie kwaheri, au nitakuwa nikikuambia kwaheri, kama mwanamke atakutuma mwambie sawa au mimi ndio nitakuwa nikikuambiwa sawa

Kama mwanamke atakuambia anakupenda mwambie mpenzi wako pia anakupenda,la sivyo nitakuambia nakutakia kila la heri 

Usicheze michezo, heshimu uhusino wetu, na naahidi tutakuwa sawa," Tansha aliweka mambo wazi.