'Mungu ni mwema naendelea vyema,'Mtangazaji Ghost Mulee azungumza baada ya kufanyiwa upasuaji

Muhtasari
  • Mtangazaji wa Radiojambo Ghost Mulee kwa mara ya kwanza amezungumza na kuwahakikishia mashabiki  kuwa anaendelea vyema baada ya kufanyiwa upasuaji
Ghost Mulee

Mtangazaji wa Radiojambo Ghost Mulee kwa mara ya kwanza amezungumza na kuwahakikishia mashabiki  kuwa anaendelea vyema baada ya kufanyiwa upasuaji.

Huku akizungumza na Gidi alisema kwamba alikuwa ameenda India kumtolea ndugu yake mkubwa figo, lakini madaktari walisema kwamba anaweza pokea matibabu bila ya kutolewa figo.

Baada ya ripoti ya daktari Ghost aliamua kufanyiwa vipimo vya mwili ambapo alipatikana na sleeping apnea.

 
 
 

Hii ni shida mbaya ya kulala ambayo kupumua mara kwa mara huacha na kuanza. Sababu za hatari ni pamoja na umri na fetma.

Ni kawaida zaidi kwa wanaume. Dalili ni pamoja na kukoroma kwa sauti na kuhisi uchovu hata baada ya kulala kamili usiku.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amewahakikishia mashabiki wake anaendelea vyema na yuko tayari kurudi nchini.

"Mungu ni mwema naendelea vyema, najaribu kutafuta njia ya kurudi Kenya," Aliandika Ghost.

Hizi hapa jumbe za mashabiki wakimtakia afueni ya haraka;

roselynevuguza: Don't worry u will find away.we miss u on radio jambo manze naomba milango ifunguke

_naomnyaboke: Usiworry coaches

 
 

tynakagasi: Worry not.. GOD in control

kachumisikachumisi: Infect we missed you in Patanisho.

kephas_official: See you soon . sir🔥🔥🔥

philipmunyawa: Pole msee. QR proud to here that u r better.❤️❤️❤️❤️

thrifty_little_decors: We miss you so much Coaches 😢