'Nakupeza sana baba,'Mbunge Mohammed Ali amuomboleza baba yake

Muhtasari
  • Mbunge Mohammed Ali amuomboleza baba yake
  • Kumpoteza umpendaye ni jambo ngumu ambalo watu wengi hawalitamani kukumbana nalo
  • Kupitia kwenye ujumbe wake Mohammed amekiri kwamba anampeza baba yake sana

Mbunge wa Nyali na aliyekuwa ripota wa Jicho Pevu Mohammed Ali kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amemuomboleza baba yake miaka 14 baada ya kifo chake.

Kumpoteza umpendaye ni jambo ngumu ambalo watu wengi hawalitamani kukumbana nalo.

Kupitia kwenye ujumbe wake Mohammed amekiri kwamba anampeza baba yake sana.

 
 

Huu hapa ujumbe wake Mohammed baada ya kupakia picha akiwa kwenye kaburi la baba yake.

"Siku yangu na baba yangu, baada ya maombi ya Eid, ni miaka 14 tangu atuache, miaka 14 nikitembelea kaburi lake na kumuombea

Wakati wa kutafakari na kukumbuka, nakupea sana baba," Aliandika Mohammed.

Hizi hapa jumbe za mashabiki wakimfariji Mohammed;

mahsin_said: Allah amrehemu na InshaaAllah amjaalie makazi yake jannatul firdaus, kisha jamani kujengea kaburi sio katika sunnah. kijiwe kinatosha

ramaohio: Moha kweli umekua mwasiasa hii Dua kwa mzee pia inataka pichapicha na camera

odhiambojosephine7919: May he continue to Rest in Peace

 
 

ocharow: Pole sana kaka

Mungu azidi kuilaza roho yake mahali pema peponi.