WAJUE WASANII

Wasanii mashuhuri wasiotokea jamii wanayojitambulisha nayo

Wasanii saba ambao kwa mara mingi wamedhaniwa kutokea jamii tofauti na lao

Padi Wubonn
Padi Wubonn
Image: Facebook

‘Mogaka’

Alikuja kutambulika sana kutokana na jukumu lake kwenye kipindi cha Vitimbi kilichokuwa kinaonyeshwa kenye runinga ya KBC. Wengi humdhania kutokea pande za Kisii kwa kuwa alijitambulisha na ameendelea kujitambulisha kama ‘Mogaka’ ambalo ni jina la Mkisii.

Lafudhi yake nzito ya Kikisii anayoitumia jukwaani pia imewafanya wengi kuamini kuwa ni mzaliwa wa jamii hilo la upande wa Nyanza Kenya. Ingawa inaaminika kuwa Mogaka alikuwa mkaazi wa mji wa Sotik kwa muda, jina lake halisi ni Francis Njenga akiwa katokea jamii ya Wakikuyu.

Dr Ofweneke

Anajulikana kwa lafudhi yake ya Kinaija ambayo ameinoa vizuri hadi wengi wakaamini kuwa ametokea nchi ya Nigeria. Hata hivyo, Sande Bush ni mzaliwa wa Nairobi kwa wazazi toka jamii ya Waluhya.

Bush amelelewa jijini Nairobi wala sio Nigeria kama baadhi ya mashabiki wake wanavyodhania.

Mogaka pamoja na Nyasuguta
Mogaka pamoja na Nyasuguta
Image: Twitter

Inspekta Mwala

Kwa mara mingi Wakenya wamemchukulia mcheshi David Mwabili almaarufu kama Inspekta Mwala kuwa wa kutokea jamii ya Wakamba.  Kwa kawaida, Mwabili amekuwa akitumia lugha iliyojaa lafudhi nzito ya Kikamba katika usanii wake.

Hata hivyo, mcheshi huyo ambaye pia ni mtangazaji wa redio Citizen amekiri kuwa anaitumia lafudhi ya Kikamba kazini tu ila kazaliwa kwenye jamii ya Wataita upande wa Pwani. Mwabili alikuja kutambulikana kutokana na kipindi cha Vitimbi na Inspekta Mwala.

Captain Otoyo Sibuor

Bwana Kazungu Matano, ambalo ni jina lake rasmi ni mzaliwa wa Pwani kwa wazazi wa jamii ya Wadigo. Kwenye sanaa yake ya ucheshi hata hivyo, Kazungu amejitambulisha kana kwamba yeye ni wa jamii ya Waluo tokea pande ya Nyanza.

Mcheshi huyo ambaye pia ni mtangazaji ni mzaliwa wa Mombasa kisha kulelewa pande ya Nakuru.

Padi Wubonn

Anajulikana sana kupendelea lafudhi ya Kiluhya. Kwenye michezo yake mingi mitandaoni, Padi hujitambulisha kama  mluhya kutokana na lugha na tabia anazoigiza.

Ingawa machache yanajulikana kuhusu maisha yake mcheshi Padi Wubonn, duru za kuaminika zimedhibitisha kuwa msanii huyo ni mwenyeji wa Nairobi akitokea jamii ya Wakikuyu.

Ondiek Nyu Kakwota

Mcheshi Hiram Mungai ajulikanaye kwa jina la usanii kama Ondiek alitambulikana miaka mingi iliyopita kupitia kipindi cha vioja mahakamani kwenye runinga ya KBC.

Kwenye michezo yake, Mungai anajitambulisha kama kwamba ametokea jamii ya Wajaluo kutokana na jina na lafudhi anayotumia kwenye mazungumzo yake. Hata hivyo, ni Mkikuyu tokea pande ya Murang’a.

Kwa sasa Ondiek anaendelea na kutumbuiza mashabiki akiwa kwenye kipindi cha Hulabaloo Estate kinachoonyeshwa kwenye stesheni ya runinga ya Maisha Magic East.

Mzee Ojwan’g

Ingawa aliaga mwakani 2015, wengi walimdhani Mzee Ojwan’g ambaye alikuwa mcheshi na msanii wa michezo ya kuigiza kuwa katokea jamii la Waluo. Hii ni kutokana na jina alilotumia jukwaani na lafudhi iliyosikika kwa mazungumzo yake.

Hata hivyo, jina rasmi lake ni Benson Wanjau tokea jamii la Kikuyu na mzaliwa wa pande ya Mukurweini iliyoko Kaunti ya Nyeri.

Mzee Wanjau alitambulikana kwa jukumu lake kwenye kipindi cha Vitimbi.