'Madaktari waliniambia nitaishi mpaka Machi,'Msanii Justina Syokau afunguka

Muhtasari
  • Msanii wa nyimbo za injili Justina Syokau amekuwa akivumma kwa muda baada ya kufunguka na kusema kwamba hana pesa na kwamba amekuwa mgonjwa

Msanii wa nyimbo za injili Justina Syokau amekuwa akivumma kwa muda baada ya kufunguka na kusema kwamba hana pesa na kwamba amekuwa mgonjwa.

Akiwa kwenye mahojiano msanii huyo alisema kwamba madaktari walikuwa wamemwambia kwamba ataishi mpaka mwezi wa machi 2021.

Hii ni baada ya kupata maambukizo ya ngozi.

"Sikufikiria kwamba nitaweza au kuishi, madaktari walikuwa wameniambia kwamba nitaishi mpaka Machi

Kwa maana nilifanya kazi kama muhudumu wa afya nilijua madkatari walijua kile wanasema na nikawaamini

Wakati ukiwa mgonjwa na wewe ni mtu mashuhuri ni ngumu, nakumbuka kuna wakati nilimtumia rafiki yangu picha ya ngozi yangu

Alikuja kunitembelea lakini alikuwa anafanya ni kama kila kitu nyumbani kwangu kimeambukizwaWakati wa ugonjwa wangu mtoto wangu na mfanyakazi wangu ndio walikaa nami," Alieleza Syokau.

Awali pia akiwa kwenye mahojiano Syokau alisema kwamba aliogopa kutangaza hali yake ya afya kwenye mitandao ya kijamii kwa maana aliogopa kejeli za mashabiki.