USHAURI WA MADAM BOSS

Usikubali kulipia penzi! Akothee ashauri wanadada

Mwanamuziki Akothee awawasuta wanaume maskini wanaotegemea wanawake kulipia bili zao

Muhtasari

•Akothee amewasuta wanaume maskini wanaotegemea wanawake kuwajibika kifedha

•Awaonya wanawake dhidi ya kutumia pesa zao kwa wanaume

Akothee
Akothee
Image: Hisani: Instagram

Mwanamuziki na mwana biashara mashuhuri Esther Akoth anayejulikana kwa jina la usanii kama Akothee amewasuta wanaume maskini wanaotegemea wake zao kutimiza majukumu yote yanahitaji fedha.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, msanii huyo ambaye ni mama wa wasichana watatu amewaonya wanawake dhidi ya kutumia pesa zao kwa wanaume.

"Usipoteze pesa yako ukiwekeza kwa mwanaume ambaye huoni siku za baadae naye. Weka pesa yako kwa matumizi ya maisha yako ya baadae:" Akothee amewashauri wanawake.

Mwanamuziki huyo ambaye anajitambulisha kama Madam Boss kutokana na hali yake ya kujitegemea na kutotazamia wanaume ameeleza pia kuwa likizo huwa tamu ikiwa mwanaume ndiye anayelipia.

"Wanaume wengine wanakuja na mawazo makubwa ya kibiashara na kunao wanawake wanachukua mikopo kwa ajili yao!! Halloo, madam jamaa amekuguza wapi." Akothee aliandika huku akiwashangaa wanawake wanaokubali kutumiwa na wanaume kifedha.

Mwanamziki huyo mwanzilishi wa Akothee Safaris pia amedai kuwa hamna shida mwanamke akifanya kazi ila mna shida ikiwa mwanamke anafanya kazi ilhali mume mwenzake hana kazi.

"Usikubali kununua mapenzi, ukianza kulipia mapenzi ukiwa bado miakani yako ya ishirini, utafanyaje ukishatimiza miaka arubaini na hamsini?" Akothee aliwauliza wanadada kwenye chapisho hilo.

Alionekana kusikitika kuwa kunao wanaume wa miaka hamsini ambao bado wanategemea wanwake kuwatunza.

"Babu, wapi akiba yako" aliandika kuwashangaa wanaume hao.

Siku chache zilizopita Akothee alitajwa kama baadhi wa wasanii wanawake tajiri zaidi Afrika.