Baadhi ya wanawake wanachukua mikopo kwa ajili ya waume zao-Akothee awashauri wanawake

Muhtasari
  • Msanii na mwabiashara Esther Akoth maarufu Akothee amezua mjadala mitandaoni baada ya kuwakashifu wanaume ambao wanwategema wanawake
akoth stylish 1 (1)
akoth stylish 1 (1)

Msanii na mwabiashara Esther Akoth maarufu Akothee amezua mjadala mitandaoni baada ya kuwakashifu wanaume ambao wanwategema wanawake.

Kulingana na Akothee baadhi ya wanaume wamo sawa wanawake wao wakiwalipia gharama. na kushindwa ni lini jukumu la mwanamume kumchunga mwanamke lilibadilika.

Pia aliwashauri wanawake wwe makini na yale yanaendelea duniani kwani ni jambo ambalo linachanganya.

"Wacha niwe mkweli kwako na pole zangu ikiwa imetua vibaya. Ili wewe kuchukuliwa kuwa Mwanamume katika ulimwengu wa mwanamke, lazima uwe katika nafasi ya kutoa suluhisho, Wanawake wanakusudia kukusaidia

Hakuna shida ikiwa mwanamke anafanya kazi na mwanamume hana kazi. Lakini kuna shida kubwa wakati mwanamume hana pesa na anatarajia mwanamke wake amuunge mkono kikamilifu 💪

Pili, likizo huhisi ya kimapenzi ikiwa ni mtu anayeilipa, au unafikiria nini? Ikiwa sivyo hebu kaa nyumbani tule nyumbani na tutumie pesa hizo kwa kodi yetu

Wanawake wanateseka mikononi mwa wanaume, 🤣🤣🤣🤣🤣. Wengine huja na maoni makubwa ya uwekezaji, na Wanawake wangu wapenzi wanachukua mikopo kwa wanaume wao," Alisema Akothee.

Akothee aliwashauri wanawake kuwekeza pesa zao baadala ya kutumia na mwanamume ambaye hana maono ya maisha yake mwenyewe.

"Ni hali ya kutumiana,usiwekeze pesa zako na mtu ambaye huna maisha naye weka pesa zako kwa ajili ya maisha yako ya usoni

Uko mchanga sana kununua mapenzi, ukianza kununua mapenzi katika miaka yako ya 20 je utafanya aje katika miaka yako ya 40 na 50

Baadhi ya wanaume wakiwa na miaka 50 wanatarajia wanawake wao kuwachunga, babu akiba yako iko wapi,"