Je wanaume huendelea na maisha yao haraka kuliko wanawake baada ya kuachana?

Muhtasari
  • Je wanaume huendelea na maisha yao haraka kuliko wanawake baada ya kuachana?

Mapenzi ni tamu lakini huwafanya watu waytende vitendo ambavyo havistahili huku wengine wakipata maumivu kutoka kwa mapenzi.

Kuna baadhi ambao wamepoteza maisha yao wakipigania mapenzi huku wengine wakiachwa na makovu na alama ya kuwakumbusha kile walipitia wakati mmoja walivyopenda.

Pia kuna baadhi ya wale hupitia changamoto nyingi na licha ya hayo yote mapenzi yao yanazidi kunoga kila kuchao.

 

Lakini kuna wale huachana kwa maana waliona kwamba uhusiano wao hauwezi endelea huku wengine wakiendelea na maisha yao.

Lakini je wakiachana nani huwa anaendelea na maisha haraka kuliko mwingine ni mwanamke au mwanamume.

Kulingana na uchunguzi wangu wanaume huendelea haraka kuliko wanawake wakitemana.

Ndio wataachana lakini kama mwanamke ana mtoto au watoto akili yake itakuwa kwa watoto na wala sio kutafuta mwanamume wa kuanzisha mapenzi naye.

Pia kuna wale uumizwa sana moyo hadi wanachukia mapenzi wanataka tu kulipiza kisasi kwa maana waliumizwa, huku muda wao ukienda sana na kupata hawajaendelea na maisha yao kama mwenzio.

Kuna wale huwa wanatamani kuendelea na maisha yao lakini unapata kumbukumbu za mpenzi wake wa awali zinamsumbua akilini mwake huku baadhi yao wakiamua kutoendelea na maisha yao.

Je kwa maoni yako ni mwanamume au mwanamke huendelea na maisha yake kwa haraka sana baada ya wawili hao kuachana?