Masomo ya kifedha tunayojifunza kutoka kwa janga la covid-19

Muhtasari
  • Hii ni baada ya baadhi yao kupoteza kazi na kuachwa na upweke licha yao kuwa na familia
  • Janga la corona limefunza kila mmoja jinsi ya kuweka akiba na kuwekeza pesa zao kwani, pesa ni kila kitu

Baada ya janga la corona kuripotiwa nchini mwaka jana 2020,Machi, wananchi wengi waliteseka na kupitia changamoto tofauti, huku wengine wakishindwa na maisha ya mjini na kurudi vijijini.

Hii ni baada ya baadhi yao kupoteza kazi na kuachwa na upweke licha yao kuwa na familia.

Janga la corona limefunza kila mmoja jinsi ya kuweka akiba na kuwekeza pesa zao kwani, pesa ni kila kitu.

 

Katika makala haya tunazingatia na kuangalia masomo ya kifedha tunayojifunza kutokana na janga la corona.

1. Weka akiba ya jambo la dharura

Kama watu wengi wangekuwa wameweka akiba ya jambo la dharura wengi wao hawangerudi mashambani wala kuomba mssaada kila mahali.

PIa familia zao zingekuwa tayari kukabiliana na jnga la corona.

2. Uwekezaji lazima uwe kipaumbele

Baadhi ya watu huwa hawawekezi pesa zao bali ni kutumia pesa zao ovyo ovyo huku wakisema msemo ya kwamba aijuaye kesho ni Mungu.

Kuwekeza inapaswa kuwa kipaumbele kwako kwa ajili ya maisha yako ya usoni.

 

3.Fanya bajeti

Ukifanya bajeti inakusaidia kujua na kufahamu jinsi ya kutumia pesa zako endapo umepokea malipo yako ya mwezi.

4.Usifanye uamuzi ambao utakuumiza

Kukabiliana na gharama za matibabu kwa sababu ya Covid-19 au kupoteza kazi yako kunaweza kukufanya ufanye maamuzi ya kupunguza kutokuwa na uhakika kwa wakati huu.

Hata hivyo, usipoteze maoni ya muda mrefu. Kwa mfano, kuuza mali, haitakuwa bora kila wakati kwa sababu bei hushuka chini ya hali hizi.

Badala yake, jilazimishe kutafakari tena jinsi na wapi unatumia pesa, jinsi ya kutumia kidogo na kuokoa zaidi.