NGUVU YA MWANAMKE

Mwanamuziki ampiga mateke shabiki aliyejaribu kumgusa visivyo

Wengi mtandaoni wampongeza staa wa Afrika Mashariki kwa kujisimamia kwenye tukio la kuhofisha

Muhtasari

•Vinka alikuwa anatumbuiza mashabiki nchini South Sudan

•Alijifungua mtoto mwezi wa Januari mwakani

Mwanamuziki Vinka ampiga teke shabiki
Mwanamuziki Vinka ampiga teke shabiki
Image: Hisani

Video ya mwanamuziki Veronica Luggya almaarufu kama Vinka wa Uganda akimpiga mateke shabiki moja aliyejaribu kumshika visivyo imeibua gumzo sana mtandaoni.

Vinka ambaye alikuwa alikuwa kwenye ziara ya kimuziki mjini Juba ulio Sudan ya Kusini alishambulia shabiki huyo alipojaribu kukiuka mipaka na tendo hilo la kuhofisha.

Kwenye video hiyo inayosambazwa mitandaoni, Vinka anaonekana kumshika mkono na kumpiga mateke kadhaa shabiki  huyo aliyekuwa ameunyoosha na nia ya kumgusa wakati mashabiki wengine walikuwa wakimshangilia staa wao.

Wengi mtandaoni wameonekana kumpongeza Vinka huku wengine wakisema kuwa alikuwa anajisimamia mwenyewe kwenye tukio la kudhalilishwa. Hizi hapa baadhi ya hisia walizotoa watu kwenye mtandao wa Twitter.

Vinka ambaye alijifungua mtoto mwezi wa Januari mwakani alionekana mwenye hasira kutokana na tukio hilo. Hata hivyo, tukio hilo halikumfanya mwanamuziki huyo kusitisha muziki kwani anaonekana kuendelea kuwatumbuiza mashabiki baada ya kushughulikia shabiki huyo aliyekosa nidhamu