USANII

DK Kwenye Beat ajivunia kukata uzani

Mashabiki wamempongeza msanii huyo baada ya kuonekana kafanya hatua katika kupunguza uzani mwilini

Muhtasari

•DK alitambulika sana kutokana na wimbo 'Asusu' na 'Furifuri' alizoimba 2014

•Wakenya wamekuwa wakimkejeli kutokana na mwili wake mkubwa

Chapisho la DK kwenye beat
Chapisho la DK kwenye beat
Image: instagram

Msanii wa nyimbo za kumsifu Mungu anayejulikana kwa jina la usanii kama DK kwenye beat amepongezwa na Wakenya mtandaoni baada ya kuonekana amefanya hatua kukata uzito wake.

Msanii huyo ambaye kwa miaka mingi amekuwa akikakejeliwa kutokana na mwili wake mkubwa amechapisha picha inayoonyesha mabadiliko katika mwili wake.

“Kujitolea husababisha hatua, kufika sasa hali mambo ni mazuri” DK aliandika chini ya picha aliyoweka kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Baadhi ya Wakenya ikiwemo wanamuziki mashuhuri waliendelea kumpongeza msanii huyo ambaye amekuwa akikosekana kwenye sekta ya uimbaji kwa muda sasa. Hizi hapa baadhi ya jumbe walizozitoa Wakenya.

Msanii huyo alikuja kutambulika kutokana na nyimbo za ‘Furifuri’ na ‘Asusu” alizoachilia mwakani 2014.