WIFE MATERIAL 2

Erico kurejesha 'Wife Material' miezi miwili tangu akamatwe

Ezekiel Mutua alishtaki mcheshi Eric Omondi kwa kosa la kutengeneza na kusambaza filamu zisizoidhinishwa na kuita studio zake 'Madanguro'

Muhtasari

•Omondi alionywa dhidi ya kuonyesha filamu chafu

•Aliachiliwa kwa dhamana ya Sh 50000

Eric Omondi
Eric Omondi
Image: HISANI: Instagram

Mcheshi tajika na asiyepungikiwa na drama Eric Omondi ametangaza kurejea kwa kipindi chake cha 'Wife Material' miezi mbili tu baada yake kukamatwa kutokana na kipindi kile.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mcheshi huyo ametangaza kuwa mkondo wa pili wa kipindi cha 'Wife Material' ungerejea tarehe ishirini na nne mwezi Mei.

"Tumerudi ni kama tu hatukuwa tumeenda!! Mei 24!! Kipindi cha maisha ya kikweli kikubwa zaidi Afrika charejea!!" Omondi aliandika.

Tarehe kumi na mbili mwezi mechi, Omondi alikamatwa na maafisa wa DCI siku moja baada ya kutangaza mkondo wa pili wa kipindi hicho. Mkurugenzi mtendaji wa bodi ya uainishaji wa Filamu nchini Kenya(KFCB), Ezekiel Mutua alidai kuwa Omondi alikuwa amekamatwa kwa kukiuka masharti ya filamu na michezo ya jukwaani kwa kutengeza na kusambaza filamu za 'Wife Material'.

Omondi aliachiliwa kwa dhamana ya Sh50000 na kisha akaomba msamaha kwa Ezekiel Mutua na Wakenya kwa jumla. Hata hivyo, ameonekana kutojuta baada ya kutangaza kuwa kipindi kile kingerejea.

Mutua alisema kuwa Omondi alikuwa katengeneza na kusambaza filamu zisizoidhinishwa. Tangulia kukamatwa kwake, video iliyoonyesha wanadada wakipigana kwenye klabu alipokuwa mcheshi huyo ilikuwa inasambazwa mitandaoni. Tukio ambalo lilidaiwa kusababishwa kukamatwa kwake.

Omondi wameonekana kuzozana mara kwa mara na Mutua kutokana na kipindi hicho huku akiziita studio za Omondi madanguro mwaka uliopita.Mutua alisema kipindi hicho kuwa hatari kwa watoto na kuagiza wasanii kutengeza vipindi zilizo sawa kwa kila mtu.

Kuanzia wiki iliyopita, Omondi ameonekana kutayarisha Wakenya kwa kurudi kwa kipindi hicho kwenye mtandao wa Instagram. Hizi hapa jumbe za kutangaza kurejea kwa kipindi hicho alizoandika Omondi.